Nadir Haroub Ally"Canavaro" akiwa na kocha wa timu yake ya Yanga African Dusan Kondic mara baaada ya mchezo kati yao na Simba SC kumalizika katika uwanja mpya wa TAIFA jijini Dar es salaam.....
Nadir Haroub"Canavaro", kiungo wa Moro Untd pamoja na timu ya Taifa" Taifa Stars" Nizar Khalfan pamoja na nyota chipukizi mwa wakata miwa waManungu- Turian Mtibwa Sugar Zahoro Pazi wanatazamiwa kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Vancouver whitecaps ya nchini Canada....
kwa mujibu wa wakala wa wachezaji hao anayetambulika na FIFA nchini Bw.Said Tulliy wachezaji hao wanategemea kuondoka nchini hivi karibuni,mara tu baada ya kumalizika kwa ligi ya Vodacom mwishoni mwa mwezi huuu
"kila kitu kinakwenda safi katika maandalizi ya safari yao, na wiki ijayo tunategemea kusaini mikataba nao kabla ya kuondoka" alisema Said Tulliy....
Mungu ibariki Tanzania tufanikiwe